Waziri wa mambo ya nje wa nchi ya Tuvalu Simon Kofe ametoa hotuba akiwa amesimama kwenye maji ili kufikisha ujumbe kwa uhalisia juu ya mabadiliko ya Tabianchi nchini humo.
Tuvalu ametoa hotuba hiyo kwenye mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika Glasgow Scotland.
Amesema amefanya hivyo ili kuonyesha jinsi nchi hiyo ilivyo mstari wa mbele katika mapambano ya mabadiliko ya Tabianchi.
Tuvalu amesema “Nimetoa hotuba nikiwa ndani ya maji ili kuonesha uhalisia tunayoyapitia watu wa Tuvalu ikiwemo kuathirika na mabadiliko ya Tabianchi kunakosababishwa na kuongezeka kwa kina cha maji ya Bahari na kutishia usalama wa wananchi hasa ukizingatia tupo visiwani”