Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema ongezeko la wimbi la watumiaji wa Shisha umesababisha madhara makubwa kwa jamii, baada ya baadhi watumiaji kuanza kutumia kifaa hicho kuchanganyia dawa haramu za kulevya tofauti na matumizi rasmi ya kifaa hicho.

Kwa mujibu wa DCEA kifaa cha Shisha ni halali kwa matumizi ya tumbaku lakini baadhi ya watumiaji wamekuwa wakitumia Shisha kuvutia dawa haramu za kulevya

Kamishna Msaidizi Kitengo Cha Kinga na Huduma za Jamii wa DCEA, Moza Makumbuli amefafanua kuwa matumizi ya Shisha kwenye tumbaku yanaruhusiwa kisheria na unaweza kugundua endapo kifaa hicho kitatoa mvuke badala ya moshi

Hata hivyo matumizi ya Shisha ni hatari zaidi kwa afya kwani kwa mujibu wa tafiti ni kuwa unapovuta Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta wastani wa sigara 100-200

Hitimana afunguka kumuweka benchi Wawa
Uwanja wa Jamhuri Dodoma waboreshwa