Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa ameupongeza ujio wa msanii maarufu kutoka India Sanjay Dutty, nakusema nia ya ujio wake wa kutaka kushirikiana na wasanii wa nchini itasaidia kukuza sekta ya filamu nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kitendo cha msanii huyo kuonyesha dhamira yake ya kutaka kuwapa mbinu waaandiaji wa filamu kwa kuwaunganisha na waandaaji wa filamu wa nchini India, kitaongeza tija katika sekta hiyo nchini sanjari na wasanii kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema kwa kushirikiana na msanii huyo wataangalia maeneo ya kimkakati kwa kubadirishana uwezo na hivyo kupanua wigo wa masoko kwa filamu za Tanzania

Aidha ujio wa Msanii nguli wa Filamu kutoka nchini India Sanjay Dutty unatarajiwa kuinufaisha sekta ya sanaa nchini baada ya kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuboresha maeneo mbambali ndani ya sekta hiyo.

Msanii huyo aliyewasili nchini kwa ushirikiano baina ya Serikali na Kampuni ya vifaa vya umeme ya Kilimanjaro Cables (AFRICAB) na kupata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa kitaifa amesema atatumia nafasi yake kuhakikisha sekta ya filamu hapa nchini inapiga hatua ya juu zaidi.

Akizungumza na wasanii mbalimbali wa filamu katika semina maalumu yenye lengo la kubadirishana uwezo, nguli huyo amesema mipango yake ni kushirikiana na wasanii wa hapa nchini kuandaa filamu mbalimbali jambo litaloweza kuwafanya kupiga hatua kimataifa.

Bilioni 67.6 kunufaisha vikundi vya kinamama
Azam FC kujipima kwa JKU