Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa imepanga kutoa shilingi Bil. 67.6 kama Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akikabidhi hundi ya shilingi 1,039,050,000 kwa vikundi 48 vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akikabidhi hundi hiyo Waziri Ummy amesema ni jukumu la kila halmashauri kuhakikisha katika makusanyo yake ya ndani inatoa asilimia 10 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu.

“Nitoe rai kwa vikundi vyote vinavyokabidhiwa hundi ya mikopo leo hii, muende mkazitumie fedha za mikopo kwa malengo mliyoyakusudia, nikosa la Kisheria kutumia fedha hizi kinyume na mkataba kama umeomba kwa ajili ya biashara hakikisha unafanya biashara na si vinginevyo,” Amesema Waziri Ummy.

Pia Waziri Ummy amezitaka Halmashauri kutumia wataalam wake kutoa elimu kwa vikundi vinavyotaka kukopa jinsi ya kutumia fedha hizo kwa miradi yenye tija na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kurejesha haraka ili na wengine waweze kunufaika.

Haya ndo maajabu ya madaktari bingwa wazawa
Sanjay tumaini jipya kwa wasanii wa filamu Tanzania