Mkurugenzi wa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dkt.James Makaragio, ametakiwa kufika katika ofisi ya Waziri wa Nishati January Makamba, kwa ajili ya kutolea maelezo ya kauli yake aliyosema kwamba kama meli ya mafuta haitoingia nchini ndani ya siku 15 basi kutakuwa na uhaba wa mafuta.
Hayo yemsemwa na Waziri Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika kwamba hakuna uhaba wa mafuta nchini na wala hakuna haja ya kuzua taharuki kuhusu upatikanaji wa nishati hiyo na kwamba serikali inaendelea kuchukua hatua ili kuongeza uhakika wa upatikanaji wake na unafuu wa bei.
“Kauli ya uhakika ni ya serikali, Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika, pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada,”
Ameandika Waziri Makamba wakati akijibu swali la mwanachi aliyehoji kuhusu mkanganyiko wa taarifa hizo katika mtandao huo.