Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bi Florence Khambi amesema kundi kubwa la vijana wa kike wamekuwa wakitumia dawa hizo kwa siri bila kugundulika hadi wanatumbukia kwenye uraibu.

Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha wengi wa waathiriwa wa dawa za kulevya wanaojitokeza kupata msaada wa tiba ya uraibu ni wanaume huku wanawake wakiendelea kujificha na kutokana na hofu ya kunyanyapaliwa

Bi Khambi amevitaka vyombo vya habari kuendelea kuelimisha jamii kuhusu tatizo la dawa za kulevya nchini na kutoa hamasa hususani kwa vijana wa kike walioathiriwa kwa matumizi ya dawa hizo kujitokeza kupatiwa tiba.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB, inasema kuwa theluthi moja ya watumiaji wa dawa za kulevya ni wanawake na wasichana huku wanaopatiwa matibabu ni moja ya tano kwa kuwa mifumo iliyopo inawaengua kupata tiba.

Kuvumilia sana chanzo cha uraibu
Niyonzima aingia rekodi za FIFA