Tabia ya kutozungumza unapokuwa na tatizo ni miongoni mwa sababu inayotajwa kuwachochea vijana wengi kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Mkufunzi mwandamizi wa maudhui mtandaoni Dotto Mnyadi amesema kuwa familia nyingi zimekuwa na tabia ya kutozungumza mara kwa mara na kuwaacha vijana hususani waliokuwa kwenye rika balehe kujisimamia bila miongozo ya karibu na upendo wa familia.
“Kuna tabia zisizofaa ambazo zinapaswa kubadilishwa,utakuta kwenye familia hawana muda hata wa kujua matatizo anayopitia mtu,hawaongei nini, na utakuta mtu anapitia kipindi kigumu lakini anajikaza, anasema huo ndo umwamba mwisho wa siku anapotea”
Amesema Dotto wakati akitoa mada kwenye mafunzo maalumu kwa wanahahabari kuhusu Dawa za kulevya yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini