Klabu ya Geita Gold inatatajwa kushinda mbio za kumsajili Mshambuliaji Ditram Nchimbi ‘Duma’, ambaye ataachana na Young Africans itakapofika Desemba 15.

Nchimbi anatarajiwa kuondoka Young Afruicans, kufuatia mkataba wake kutarajia kumalizika mwezi ujao, na kanuni zinamruhusu kufanya mzungumzo na klabu yoyote kwa sasa.

Taarifa zinaeleza kuwa Geita Gold ambayo inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/22, ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Mshambulaiji huyo.

Endapo taarifa za Nchimbi mwenye umri wa miaka 23 zitathibitishwa na Uongozi Geita Gold, atakuwa mchezaji halali wa klabu hiyo ya Mkoani Geita kuanzia Desemba 16, siku moja baada ya usajili wa dirisha dogo kufunguliwa.

Tayari Nchimbi alishathibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika: “Mkataba wangu na Young Africans SC unakwisha tarehe 15 Decemba 2021 saa 00:00 (Saa Sita Usiku). Kwa sasa nipo likizo mpaka mkataba wangu utakapokwisha ndio maana sipo na timu.”

“Nina ofa nyingi tu mkononi, kutoka Police, Geita, Mtibwa, Namungo na timu nyingine nyingi tu. Baada ya mkataba kwisha mtafahamu naelekea wapi.”

PICHA: Young Africans yasafiri kwa basi
Franco Pablo: Mchezo utakua mgumu