Mwanamuziki Robert Thornton Jr, maarufu Young Dolph ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya duka moja huko Memphis, Novemba 17, 2021.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ndio mmiliki wa duka aliloingia marehemu Dolph(36) amesema kuwa lilitokea gari ambalo ndani yake walikuwamo watu wawili ambao  walishuka na kumshambulia kwa risasi rapa huyo ikiwa ni majira ya saa saba mchana,  kisha kutokomea kusiko julikana.

Licha ya Meya wa jiji la Memphis Jim Strickland kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo kwa vyombo vya habari, lakini bado jeshi la polisi halijatoa taarifa rasmi juu ya undani wa tukio hilo.

Kinachoendelea kusimuliwa na mashuhuda na baadhi ya watu wenye taarifa za ndani juu wa tukio hilo akiwamo Dj Akademiks, ni kuwa rapa Young Dolph kabla ya kuuawa alikwenda dukani hapo kwajili ya kumnunulia mama yake mzazi Cookes (Vitafunwa).

Aidha kwa mujibu wa Dj Akademiks ambaye ameutumia ukurasa wake wa mtandao twitter kuelezea machache aliyoyapata kuhusu undani wa tukio hilo amesema kuwa licha ya kushambuliwa, Young Dolph alijitahidi kujibu mashambulizi ya maadui zake hao kwa kupiga risasi kadhaa, lakini hakufanikiwa kujisaidia kwa kuwa tayari alikuwa ameshambuliwa kwa risasi nyingi mwilini hali iliyompelekea kufariki Dunia.

Mnamo mwaka 2016 Dolph aliachia album yake ya kwanza ‘King of Memphis’ ambayo ilifanikiwa kuingia mpaka namba 49 kwenye chati za Billboard hot 200, na baadaye kusogea mpaka namba 35 kwenye Billboard Hot 100.

Beaumellle: Africa inaonewa
PICHA: Young Africans yasafiri kwa basi