Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara ameuagiza Wakala wa Barabara Nchini(TANROARDS) kuhakikisha wanashughulikia changamoto ya madai ya dalili za kudaiwa rushwa kwa vijana wanaoomba kufanya kazi kwenye mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Amebainisha kuwa mradi huo ni mzuri wenye manufaa kwa wananchi sababu utapunguza msongamano hivyo ukikamilika utafungua njia ya Dodoma na kuondoa upotoshaji kuwa hautafanyika.
“Mmeshalipwa asilimia 20 ya fedha hadi sasa hivyo chapeni kazi kwa mujibu wa mkataba ambao unaeleza hadi Desemba 7, 2024 uwe umekamilika hivyo mkiweza malizeni kabla ya muda. Viongozi wataendelea kuja hapa mara kwa mara sababu Serikali imewekeza fedha nyingi hivyo hakikisheni mnalipa fedha kwa kadri mlivyoingia mkataba sio kuwazungusha,” Amesema Naibu Waziri Waitara.
Mhandisi Chimagu amesema kuwa kiasi cha sh. bilioni 12.47 zimelipwa kama fidia kwa wananchi 2.388 waliopisha mradi ambapo kati ya hao 470 waliobaki wanaendelea kulipwa sababu fedha zimeshatolewa wiki iliyopita.