Uongozi wa klabu ya Juventus ya Italia umeanza mazungumzo na beki wao wa kati, Matthijs de Ligt kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya ambao utafikia tamati mwaka 2025.

De Ligt msimu huu amejikuta akiwa anawekwa nje mara kwa mara na wakongwe Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini.

Oktoba, mwaka huu alikiri kuwa hana furaha na nafasi anayopata klabuni hapo, huku akihusishwa na kuhamia katika klabu za Barcelona na Chelsea.

Ingawa kuna uvumi huo, lakini Juventus hawana mpango wa kumwachia huku wakizipuuzia taarifa za wakala wake, Mino Raiola.

Mkataba wa sasa De Ligt na Juventus unamalizika mwaka 2022, huku kukiwa na kipengele cha euro milioni 150 kama ada ya kuvunja mkataba.

Nchimbi asajiliwa Geita Gold FC
Bilioni 450 hugharamia mafuta ya kula kila mwaka