Katika kuazimisha miaka 60 ya Uhuru Uongozi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere umewashauri vijana kuacha kujipendekeza kwa viongozi badala yake wakosoe na kutoa ushauri pindi wanapoona mambo hayoko sawa

Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Steveni Wasira, amesema vijana wananafasi kubwa katika kuleta maendeleo.

”Unawezaje kumfanya mtu awe mzalendo asiyeijua nchi yake, maana uzalendo ni kuijua kwanza nchi yako na pili kuipenda sasa wewe unapenda nchi usiyoijua unapendaje usichokijua, kwahiyo nadhani Challenge ipo kwa nchi yetu kwamba tuanze sasa kudirect mafunzo yetu kuanzia shule za msingi ili kujenga uzalendo wa kweli” amesema Wasira

Naye kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kumbukmbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila, amesema elimu ya Uongozi na maadili itasaidia viongozi kufikisha uogozi kwa wananchi.

”Ngongamano hili amablo tumelifanya leo linakauli mbiyo isemayo Uongozi na maadili katika miaka 60 ya Tanzania bara, ni kuumbushe jamii kuwa chuo hiki kina historia ambayo huwezi kuitenganisha na historia ya uhuru wa Tanzania bara chuo hiki kilianzishwa miezi minne tu baada ya kupata Uhuru” amesema Prof. Mwakalila

Kwa kupitia amfunzo haya ya Uongozi na maadili ambayo tunayatoa basi tunategemea kwamba taifa litapata viongozi ambao ni waadili waamini ambao kwakweli wanaweza wakaendeleza hizi tunu za taifa na hii misingi iliyojengwa na waasisi wa Taifa hili”amesema Prof. Mwakalila

Rais Samia kuwatunuku Kamisheni JWTZ
Museveni awataka waasi wa ADF kujisalimisha