Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali ili kuboresha biashara, mazingira na  uwekezaji.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi. Robert Gabriel, wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Ukwaju katika Wilaya ya Nyamagana.

Mhandisi Gabriel, amesema kuwa Serikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha Saccos kwa ajili ya kuwakopesha machinga na kuwawezesha kuboresha biashara yao,mazingira ya biashara na uwekezaji.

“Bado mambo kadhaa yanafanyika na baada ya wiki chache tutafungua Machinga Saccos, kinachosubiriwa ni utaratibu.Tunawafahamu machinga wanaofanyabiashara hapa ili fedha hii tunayowakopesha isipotee lazima tuwahakiki tuwe na taarifa kibanda hiki anakimiliki nani apewe mkopo,”amesema Mhandisi.Gabriel.

Mkuu huyo wa mkoa aaaameeleza kuwa fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri  kwa wajasiriamali bila riba,itatolewa kwa mkakati kwa wanawake, walemavu na vijana wanaofanyabiashara kwenye masoko rasmi.

“Hatuwezi kusema tunawapanga halafu ana kuja mtu anachukua maeneo kwa majina tofauti,haki na kweli lazima visimame na machinga waheshimiwe,”amesema Mhandisi.Gabriel.

Aidha, amesisitiza kuwa machinga wasipoteze fursa ya kupata mikopo isiyo na riba, hivyo wapewe elimu wapate mikopo hadi waikimbie lakini wakumbuke kurejesha.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Sekiete, amesema elimu itaanza kutolewa kabla ya machinga kupata mikopo hiyo isiyo na riba lakini amesema ipo changamoto ya baadhi ya machinga kurudi kupanga bidhaa na kufanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi walikoondolewa kutokana na wafanyabiashara wakubwa kutoa bidhaa kwa wafanyabiashara hao wadogo.

Waziri Mkuu kurejeshwa madarakani
Rais Samia awasili mkoani Arusha kwa ziara ya siku tatu