Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe, amewataka wananchi kuacha tabia ya uharibifu wa mazingira na kusingizia mabadiliko ya tabia nchi.
Ameyasema haya leo Novemba 21, 2021 katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya mvuvi duniani iliyofanyika katika mkoani Kigoma.
Amesema nchi ipo kama ilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu ila shughuli za kibinadamu za ukataji miti na uharibifu mwingine wa mazingira ndio hasa chanzo cha kuiharibu nchi.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa makusudi kwa kuwa jambo hilo litazidi kuharibu mazingira na kuteketeza rasilimali zilizopo.