Mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel Gabriel ‘Batgol’amemtaja Mshambuliaji kutoka DR Congo Chriss Mutshimba Koppe Mugalu, kwa kusema ndiye Mshambiliaji anayefuata nyayo zake ndani ya kikosi hicho.
‘Batgol’ aambaye kwa sasa ni meneja wa kikosi cha Mbeya Kwanza FC, amesema sifa kubwa inayompa nafasi Mugalu hadi kumfikiria huenda akawa na sifa alizokua nazo, ni uwezo wake wa kupambana na kujua namna ya kuwaadhibu wapinzani.
Amesema kwa sasa kwenye kikosi cha Simba SC kuna Meddie Kagere na Mugalu wote ni wapambanaji mmoja akiwa mviziaji na mwingine ana uwezo wa kutafuta na kufunga.
“Nimekuwa nikifananishwa na Kagere ni kweli tunaweza kufanana vitu vichache si vyote kwani mimi nilikuwa nacheza nafasi hiyo kwa kuwa na uwezo wa kufunga na kutafuta mipira kwa kusumbuana na mabeki kama ilivyo kwa Mugalu lakini Kagere yeye anaweza kuvizia na kufuynga,”
“Uwezo wangu kwa kweli ninaufananisha na Mugalu kwa sababua na kila vigezo ambavyo niliwahi kuvitumia na kuiwezesha Simba SC kupata mafanikio katika kipindi chote nilichokua Msimbazi.”
Mugalu alisajiliwa Simba SC msimu uliopita akitokea Lusaka Dynamos FC ya Zambia, na alimaliza msimu akiwa nafasi ya pili katika nafasi ya ufungaji Bora akitanguliwa na John Raphael Bocco.