Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amepokea Vifaa vya Usafi ikiwemo Vifaa vya kuhifadhi taka na Fagio kutoka kwa Jumuiya ya Mabohora Kama sehemu ya kuunga mkono Kampeni ya Kusafisha na Kupendezesha Dar es salaam.
Akipokea Vifaa hivyo RC Makalla amewashukuru Mabohora kwa kutekeleza ahadi waliyoitoa Wakati wa Uzinduzi wa Mkakati endelevu wa Usafi Uliofanyika November 22.
RC Makalla amesema katika kuelekea Uzinduzi wa Kampeni hiyo Jumamos ya Disemba 04, Maandalizi yote yamekamika na kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza kufanya Usafi wa pamoja kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora, Murtaza Adamjee amesema Jumuiya hiyo ipo bega kwa bega na RC Makalla kufanikisha Kampeni hiyo.