Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa Ardhini LATRA kurejesha Kituo Cha Daladala Cha Buguruni Kama awali ili kuchochea Biashara kwenye Soko la Buguruni.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Malalamiko yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Soko Hilo na baadhi ya Viongozi waliodai Kituo hicho kilisimama kwa sababu zisizoeleweka.
Kutokana na hilo RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuongozana na LATRA Disemba 6, Hadi kwenye Kituo hicho ili kukamilisha taratibu za kurejesha Kituo hicho.
Aidha RC Makalla amewaelekeza TARURA kufika eneo la Buguruni na kufanya taratibu za maboresho ya Barabara za kuingia na kutoka sokoni apo ili ziendane na hadhi ya Soko.
Hayo yote yamejiri wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi na Maboresho ya Soko la Kisasa Buguruni.