Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamerejea nyumbani Dar es salaam-Tanzania Bara, wakitokea Lusaka-Zambia walipokwenda kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya mtoano dhidi ya Red Arrows.

Simba SC wamewasili Dar es salaam, wakiwa na kazi kubwa ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans ambao utapigwa Jumamosi (Desemba 11) Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini humo.

Hata hivyo tayari kikosi cha Mabingwa hao kilianza maandalizi ya mchezo huo jana Jumatatu (Desemba 06), kikiwa mjini Lusaka-Zambia.

Simba SC imefuzu kucheza hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa 4-2 dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Katika Mchezo wa Mkondo wa Pili uliochezwa Jumapili (Desemba 05), wawakilishi hao wa Tanzania walikubali kupoteza kwa kufungwa 2-1, Uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka-Zambia.

Uswizi yaidhinisha Kifaa cha kujiua
Simba SC yaigomea GSM