Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ limeifungia klabu ya Sofapaka FC ya Kenya kutofanya usajili wa wachezaji wa kimataifa na kuliomba shirikisho la soka la Kenya ‘FKF’ kuizuia timu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani kwa kushindwa kulipa madeni wanayodaiwa na mchezaji wao wa zamani.

Hatua hiyo imekuja baada ya miamba hiyo kusitisha mkataba na mshambuliaji kutoka Ghana, Jedinak Nana Ameyaw kwa “muendelezo wa kiwango kibovu”.

Sofapaka ilisitisha mkataba wa mchezaji huyo mwezi Januari mwaka huu 2021.

Mchezaji huyo aliyekuwa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo alikata rufaa kupitia Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa cha Ghana akitaka alipwe mishahara ya muda uliosalia katika mkataba wake.

Kwa mujibu wa FIFA, dhabu iliyowasilishwa kwa Sofapaka Jumatatu (Desemba 06) itakoma pale tu mchezaji huyo atakapolipwa stahiki zake.
Rais wa klabu hiyo Elly Kalekwa amenukuliwa na BBC akisema: Tuna kila aina ya dhamira ya kumlipa fedha zake haraka iwezekanavyo.

Kinachokwamisha ni changamoto ya fedha tuliyonayo kwa sasa”.
Kalekwa ameongeza kuwa klabu hiyo inatarajai kumalizana na deni hilo ifikapo Jnuari mwaka 2022.

Ameyaw anaidai Sofapaka FC $12,000 (TZS 26m) za mshahara wa mwaka mmoja na nyongeza ya $1,000 (TZS 2m) za gharama za kisheria.

Makubaliano ya Biden na Putin hayafikia muafaka
Lori laua wanafunzi wawili