Gwiji wa soka nchini Brazil, Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ amelazwa hospitali akisumbuliwa na matatizo ya uvimbe kwenye utumbo mpana.

Dakati wa Hospitali ya Sao Paulo, Albert Einstein, amethibitisha taarifa za Gwiji huyo mwenye umri wa miaka 81 kulazwa hospitalini hapo.
Einstein amesemaPele yuko katika hali nzuri na ataruhusiwa katika siku chache zijazo.

“Pele sasa anaendelea vizuri na matibabu yake.” amesema daktari huyo
Mwezi uliopita Pele aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter “Nina afya njema na ninajihisi kuwa bora kila siku, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Septemba.”

Pele alikuwa akitibiwa hospitalini hapo tangu Agosti 31 baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida.

Afya yake imekuwa ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni na alifanyiwa upasuaji wa tezi dume mwaka 2015 baada ya kulazwa kwa mara ya pili ndani ya miezi sita. Alilazwa tena kwa maambukizi ya mkojo mwaka 2019.

Pele ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa amefunga mabao 77 katika michezo 92 na mmoja wa wachezaji wanne pekee waliofunga katika michuano minne ya Kombe la Dunia.

Mabeki Young Africans wakabidhiwa jukumu zito
Watu 53 wafariki kwa ajali