Ni wiki chache tu tangu kuchangisha kiasi cha pesa kisichopungua Naira 250,000,000. Sawa na Shilingi Bilioni (1,401,433,650.75) za Kitanzania, alizozikusanya kwa kuanzisha kampeni maalum mtandaoni na kuzipeleka kwenye vituo vya watu wenye uhitaji maalumu kama sehemu ya kurejesha kwa jamii katika siku yake ya kuzaliwa.

Hatimaye mwanamuziki David Adeleke Adeleji maarufu Davido amejinunulia zawadi maalumu kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya Krismasi.

Zawadi hiyo gari la kifahari aina ya Lamborghini Aventador lenye thamani ya $550,000 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 1,266,650,000 za Kitanzania.

Kabla ya hapo Davido mwanzoni mwa mwaka 2021 alifanikiwa kununua gari jingine la thamani aina ya Roll Royce Cullinan lenye thamani ya $500,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,151,500,000 za Kitanzania.

Kutokana na thamani ya vitu anavyomiliki msanii huyo yakiwamo magari hayo ya kifahari, Davido anaendelea kujikita kwenye nafasi za juu miongoni mwa wasanii wenye uwezo mkubwa barani Afrika.

Kanye na Drake wamsaidia Kiongozi wa Genge la uhalifu
Utekelezaji kampeni kabambe ya mazingira yapamba moto