Usiku wa kuamkia leo Desemba 10, 2021 Kanye West na Drake walitumbuiza pamoja kwenye tamasha la hisani ili kumsaidia Larry Hoover, kiongozi wa zamani wa genge la kihalifu ambaye amekuwa akitumikia kifungo jela kwa miongo kadhaa sasa.

Wawili hao walitumbuiza pamoja katika ukumbi wa Los Angeles Memorial Coliseum siku ya Alhamisi usiku dhamira ikiwa kukusanya kiasi cha pesa kitakachotumika kumsaidia Larry Hoover kutoka gerezani..

Larry Hoover  mwenye umri wa miaka 71, ni mmoja wa viongozi wa genge la Chicago liitwalo Gangster Disciples lililotamba sana kati ya miaka ya 1970 na 1995.

Alipatikana na hatia za kuamuru mauaji na alikuwa gwiji wa biashara ya dawa za kulevya mnamo mwaka 1973 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 150-200.

Maduka yapigwa marufuku kutoa ushauri
Davido ajinunulia gari la kifahari kama zawadi ya Krismas.