Mwanamuziki Nyamari Ongegu maarufu Nyanshiski amefunga ndoa na mpenzi wake Zia Bett katika hafla ya faragha iliyofanyika mapema leo Desemba 10, 2021 ikiongozwa na mchungaji Nick Korir wa Nairobi Chabel.

Nyanshiski na mkewe walikula Kiapo mbele ya kikundi kidogo cha familia na marafiki wa karibu huko Nairobi Kenya.

Ambapo nyota huyo alisindikizwa na mastaa kadhaa akiwamo aliyekuwa mshirika wake mkubwa kwenye Band yake Kleptomaniax, Dj Stylez, Big Pin, pamoja na Wahu.

Huku nafasi ya mpambe wake ikishikiliwa na meneja wake wa zamani ambaye kwa sasa ni mtayarishaji wa Filamu maarufu nchini humo Fakii Liwali pamoja na masanii Nameless.

Mwishoni mwa mwaka 2019, wawili hao walifanya sherehe ya kitamaduni iliyowavutia wengi huko katika Kaunti ya Nandi ambayo ilihudhuriwa na familia, marafiki wa karibu, pamoja na watu mashuhuri kutoka maeneo tofauti tofauti.

Nyanshiski na Zia Bett ni wapenzi wa muda mrefu ambao wamechagua kuyaweka mahusiano yao yaliyodumu kwa kipindi kirefu nje ya umaarufu wao, huku wakiwa wamebarikiwa kupata mtoto mmoja.

Bashungwa: Vyama vya michezo tumieni Taifa CUP
Maduka yapigwa marufuku kutoa ushauri