Mwekezaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ amethibitisha kupokea maoni ya kujenga Uwanja kutoka kwa Mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Pendekezo la kujengwa kwa Uwanja wa Simba SC, lilitolewa jana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Crescentius Magori alipompa pole Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez kufuatia sakata la kuzuiwa kuingia Uwanja wa Mkapa Jumamosi.

‘Mo’ amethibitisha kupokea maoni hayo kwa kuandika ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

‘Mo’ ameandika: Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo. Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili.

Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji. Kwa kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba wanasimba tuchangie sote.

Kwa sasa klabu ya Simba SC inamiliki Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju, Dar es salaam wanaoutumia kwa mazoezi.

Angetile amshangaa kiongozi Biashara United Mara
Bulembo bampa tu bampa na Polepole