Watu 9 wamefariki dunia ikiwemo wanawake 4 na wanaume 5 na wengine 3 kujeruhiwa baada ya Gari ya magazeti aina ya Toyota Hiece mali ya Kampuni ya Soma General Traders iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya yenye usajili namba T249 DWT kupata ajali.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Alan Bukumbi amesema kuwa gari lilimshinda dereva kwenye Kona kuacha njia, kugonga mti na kusababisha ajali hiyo.

Aidha Kamanda Bukumbi amesema majeruwi wamepelekwa hospital wakipata matibabu ingawa Hali zao Bado sio nzuri, huku miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Iringa

Rais Mwinyi ateta na kamati ya maadili
Rais Ramaphosa akabidhi majukumu yake