Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka Uongozi wa Tume ya Maadili ya viongozi wa Umma kujiridhisha ili kubaini sababu za msingi za Viongozi 52 kushindwa kurejesha Fomu za Tamko la Rasilimali na madeni kwa wakati uliowekwa  na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria.
 
Dk. Mwinyi ametoa wito huo leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakili, Kikwajuni Jijini Zanzibar.
 
Amesema katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 jumla ya Viongozi 2578 walichukua Fomu za tamko la Rasilimali na madeni ambapo Viongozi 2556 walirejesha fomu hizo  kwa wakati muafaka, huku Viongozi 52 wakirejesha  fomu hizo nje ya muda uliowekwa.
 
Amesema viongozi waliorejesha fomu hizo nje ya wakati uliowekwa ni namna ya viongozi  wanaopewa kazi na kuacha kuzifanya na pale inapotokea wakafanya  hukamilisha kwa wakati wanaopenda wao wenyewe.
 
Dk. Mwinyi amewakumbusha Viongozi wote wa Umma waliotajwa katika sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuhakikisha wanarejesha Fomu hizo baada ya kuzijaza sio zaidi ya tarehe 31 Disemba, 2021.

Rufaa ya Sabaya na wenzake kusikilizwa Februari 14, 2022.
Tisa wafariki Dunia