Mahakama Kuu Devisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayohusu maelezo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, Mohamed Abdillah Ling’wenya, kufuatia pingamizi lililowekwa na mawakili wa mshtakiwa huyo, Fredrick Kihwelo na Dickson Matata.

Katika kesi hiyo ndogo mawakili hao wa mshtakiwa huyo walipinga kupokewa maelezo hayo akitoa hoja mbalimbali huku akiungwa mkono na mawakili wengine wa utetezi.

Mawakili wa utetezi walipinga kupokewa maelezo hayo kwa madai kuwa mshtakiwa huyo hakutoa maelezo kituoni hapo, kwa kuwa hajawahi kufikishwa kituoni hapo na kwamba hakuwahi kutoa maelezo yake popote.

Mapingamizi hayo yametupiliwa mbali leo Jumanne Desemba 14, 2021 na Jaji Joachim Tiganga ambaye amesema hoja zote za utetezi zimetupiliwa, ambapo Mahakamainaendelea kusikiliza kesi ya msingi kwa shahidi wa Jamhuri SP Jumanne Malangahe kuendelea ushahidi wake Mahakamani.

Rais Mwinyi afanya uteuzi
Waziri aweso awapa maagizo maafisa ugavi