Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Young Africans Rodgers Gumbo amesema klabu hiyo ina nafasi ya kusajili wachezaji wengine wawili wa kimataifa kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo Januari 15/2022.
Msimu wa Dirisha Dogo la usajili 2021/22 umefunguliwa rasmi leo Jumatano (Desemba 15) kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kufanya usajili.
Gumbo amesema kamati yake ifafa nikisha usajili kwa matakwa ya Benchi la Ufundi, hivyo Mashabiki na Wanachama wa Young Africans waendelee kusubiri.
“Kuhusiana na usajili wa nyota wa kimataifa hatutarajii kufanya mabadiliko makubwa sana ya kikosi kwenye dirisha hili dogo la usajili.” Amesema Gumbo
“Tuna nafasi mbili lakini mpango wetu ni kusajili mchezaji mmoja tu ambaye atakuja kuziba pengo la Yacouba Songne, ambaye ripoti za kitabibu zinaeleza atakuwa nje mpaka mwishoni mwa msimu.”
“Hivyo tunatarajia kusajili kiungo mmoja mshambuliaji, kuhusu usajili wa Chama hilo liko chini ya kocha wetu mkuu Nasreddine Nabi, ambaye alipata nafasi ya kumuona Chama akicheza hapa nchini na kama ataona hilo ndilo chaguo sahihi la kuziba nafasi ya Yacouba basi tutahakikisha tunamsajili.”