Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Maketi Msangi amefafanua tukio la kudondoka kwa Ndege katika ziwa Victoria takribani mita 500 kutoka barabara za kuruka na kutua ndege.

Akizungumza na Dar24Media Kaimu Kamanda Msangi amesema kuwa baada ya kupata taarifa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama wakiwemo askari maji walifika eneo la tukio wakiwa na boti mbili za uokozi pamoja na magari ya kubeba majeruhi yaliyokuwa yamepaki kando ya uwanja.

Amesema kuwa baada ya kufika walikuta kuwa ni tukio la kutengenezwa lililofanyika kwa mjubu wa taratibu na sheria za anga huku akisema wao kama jeshi waliendelea na utaratibu wa uokozi na kuokoa watu 23 kwa mafanikio.

Hata Kaimu kamanda amesema zoezi hilo mamlaka a anga imelifanya ili kuona namna gani vyombo vya usalama viko tayari kukabilia na majanga kama hayo endapo yakitokea.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 16, 2021
Waziri Ummy akemea utozaji wa michambo kwa wanafunzi