Serikali imepiga marufuku wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwashusha vyeo walimu wakuu wa shule pindi shule zao zinapopata matokeo mabaya.
Marufuku imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, wakati akifungua mkutano wa wakuu wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Waziri Ummy amesema inashangaza kuona walimu wakuu wakishushwa vyeo kiholela na wakurugenzi kila shule inapofanya vibaya wakati mwalimu huyo hajawezeshwa.
“Walimu mmekuwa msaada mkubwa sana kwa maendeleo ya elimu lakini hii tabia ya kuwaonea kwa kuwashusha vyeo imeshamiri na siikubali. Sasa kuanzia sasa sitaki kusikia tabia hii nitawalinda walimu wangu dhidi ya unyanyasaji wa mtu yeyote,” alisema Mhe. Ummy.
Mkurugenzi unapomvua madaraka Mkuu wa shule je yeye ametekeleza majukumu yake amemuwezesha Mkuu wa shule hiyo ipasavyo; Naomba kwa pamoja tushirikiane katika kuboresha matokeo ya wanafunzi na sio kuadhibiwa mtu mmoja tu.