Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuanza mchakato wa kutafuta Kiungo mpya atakayechukua nafasi ya Kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba, wakati wa Dirisha Dogo la Usajili.

Manchester United inatajwa kwenye orodha ya klabu zitakazofanya usajili nchini England wakati wa Dirisha Dogo mwezi Januari 2022, ili kuboresha kikosi chake.

Pogba mwenye umri wa miaka 28, amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake Old Trafford, na bado hajasaini mkataba mpya, jambo ambalo huenda likamfanya aondoke kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Telegraph, Manchester United itaelekeza nguvu kunasa kiungo wa Olympic Marseille ya Ufaransa Boubacar Kamara.

Mwingine anayetajwa huenda akasajiliwa na Manchester United kama mbadala wa Pogba ni Kiungo wa Aston Villa John McGinn na nyota wawili wa RB Leipzig Amadou Haidara na Christopher Nkunku ambao wote wamekuwa wakihusishwa na miamba hiyo ya Old Trafford siku za karibuni.

Aubameyang kutua FC Barcelona
Bunge lapitisha matumizi ya BANGI