FC Barcelona inatajwa kuwa kwenye mpango wa kusamjili Mshambuliaji kutoka nchini Gabon na klabu ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang.
FC Barcelona inatajwa kuwa kwenye mpango huo, ili kuziba nafasi ya Sergio Kun Aguero aliyetangaza kustaafu soka jana Jumatano (Desemba 15), kufuatia matatizo ya moyo yanayomkabili.
Aubameyang amekuwa chaguo la kwanza kwenye orodha ya Washambuliaji wanaotajwa huko Camp Nou, kutokana na uzoefu alionao, hasa baada ya kucheza katika Ligi ya Ufaransa, Ujerumani na England.
Taarifa zinaeleza kuwa, FC Barcelona huenda wakatuma Ofa Kaskazini mwa Jijini London yalipo Makao Makuu ya Arsenal, wakati wa Dirisha Dogo la Usajili ambalo rasmi litafunguliwa mapema mwezi Januari 2022.
Aubameyang yupo kwenye mazingira tatanishi kwenye kikosi cha Arsenal, kufuatia tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili katika kipindi hiki, huku Meneja Mikael Arteta akimvua unahodha.
Mkataba wa sasa wa Aubameyang na Arsenal utamalizika 2023.