Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza MZFA kupitia kamati ya Mashindano, imeteua Kamati ya Tuzo na Zawadi kwa msimu 2021/2022.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Katibu Mkuu wa MZFA Leonard Malongo amesema wameamua kuteua Kamati hiyo Ili iratibu Tuzo za Msimu huu kwa weledi na ufanisi mkubwa.
“Kamati ya Mashindano ya MZFA pamoja na kupitia mwendelezo wa ligi ya Mkoa inayoendelea imeamua kuteua Kamati ya Tuzo na Zawadi Ili kukasimu madaraka ya uratibu utoaji wa tuzo” Alisema Malongo.
Malongo ameitaja Kamati hiyo ambayo inaundwa na watu tisa kuwa ni –
- Juma Kitenge – Mwenyekiti
- Fabian Fanuel- Katibu
- Rashid Ratto Mjumbe
- Francis Felician – Mjumbe
- John Tegete – Mjumbe
- Abdallah Chaus – Mjumbe
- Ibrahim Mulumba – Mjumbe
- Sebastian Rehani – Mjumbe
- Godfrey Chapa – Mjumbe
Malongo ameipa baraka Kamati ya Tuzo Kuanza kazi yake mara moja ili kukimbizana na mwenendo wa uratibu na utoaji wa tuzo msimu huu kwa vipengele Mbalimbali vya tuzo za Msimu huu.
Katibu wa Kamati ya Tuzo Ndugu Fabian Fanuel ameishukuru MZFA kwa kuiamini Kamati teule ya tuzo na zawadi, na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote Ili kufanikisha zoezi hilo.