Imefahamika kuwa maamuzi ya Uongozi wa klabu ya Young Africans kutarajia kumpeleka Shomari Kibwana nje ya nchi kwa ajili ya matibabu, yametokana na msukumo kutoka kwa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Taarifa za Kibwana kuwa majeruhi zilithibitishwa jana Alhamis (Desemba 16), kupitia taarifa maalum iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu hiyo.

Kocha Nabi amesema alilazimika kuwataka viongozi kumpeleka nje ya nchi beki huyo kiraka kama walivyofanya kwa Mshambuliaji Yacouba Sogne, ili aweze kupata matibabu ya haraka na kurudi katika hali yake ya kawaida.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema, anaamini beki endapo atapata nafasi ya kutibiwa nje ya nchi, atakua na nafasi ya kupona haraka na kurudi katika majukumu yake.

“Nimewaomba viongozi wampeleke Kibwana nchini Tunisia sehemu aliyopelekwa pia Yacouba kwa ajili ya matibabu zaidi ya kina, kwani kule ni mahali tulivu na penye mazingira rafiki,” amesema Nasreddine Nabi.

Kibwana aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC uliochezwa Jumamosi (Desemba 11), Uwanja wa Benjamin Mkapa na timu hizo kutoka suluhu.

Young Africans yaanza safari
Young Africans yatumiwa salamu