Kikosi cha Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans kimeanza safari ya kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kupitia mkoani Mbeya.

Young Africans imeondoka jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Desemba 17) Mchana kwa usafiri wa Ndege, na itakapofikwa mkoani Mbeya itatumia usafiri wa basi kuelekea mjini Sumbawanga tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa tisa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Young Africans itacheza dhidi ya Tanzania Prisons Jumapili (Desemba 19), katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Hata hivyo katika Msafara huyo, wachezaji wanne wameachwa jijini Dar es salaam kutokana na kuwa majeruhi, akiwamo beki kiraka Kibwana Shomary.

Mbali na Kibwana, wengine waliobaki Dar es salaam ni Yacouba, Yusuf Athuman na Mapinduzi Balama.

Meneja wa Young Africans Hafidh Saleh amesema wengine waliosalia wapo fit akiwamo Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele, ambaye juzi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Ihefu aliishia kukaa jukwaani.

Young Africans itavaana na Tanzania Prisons huku ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na alama 20, huku Tanzania ikiwa nafasi ya 13 kwa kumiliki alama 8.

Simba SC wasubiri baraka za Kocha Pablo
Nabi afunguka matibabu ya Kibwana Shimari