Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji.

Akisoma hukumu hiyo, baada ya kusikiliza upande wa Kamati na Upande wa Utetezi, Mwenyekiti wa Kamati, Habbi Gunze amesema maudhui ya kipindi cha shule ya uongozi yalikuwa ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

Kamati imesema kuwa kituo kimevunja kanuni na maadali ya uandishi na utangazaji kwa kutowapa nafasi viongozi aliowatuhumu ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma alizotoa ni pamoja na tuhuma ya “Kuhusu kuwapanga wamachinga, Humphrey Polepole Online TV iliwatuhumu viongozi wa Serikali kuhusu kutofuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ya kuwapanga vizuri wamachinga.

Aidha kamati imejiridhisha kuwa Polepole TV imekiuka sheria za mawasiliano kwa njia ya kieletroniki, na kutoa onyo kali kwake, lakini pia kukifungia kipindi cha Shule ya uongozi kwa muda mpaka pale atakapofanya aliyopangiwa na kamati hiyo.

Mambo aliyopangiwa na kamatyi hiyo ni pamoja na Kuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi wa habari na utangazi na kuleta tija na ufanisi katika vipindi vyake, Kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, misingi na kanunia za uandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake.

Waziri Jafo ateta na NGOs
Afufuka baada ya miaka 4 ya kifo