LIGI Kuu ya England (EPL), itaendelea na ratiba yake kama kawaida licha ya mlipuko mpya wa virusi vya corona na kusababisha michezo kadhaa kuahirishwa.
Ilitarajiwa huenda michezo itakayochezwa baada ya Sikukuu ya Krismas ingehairishwa, lakini hakuna kura iliyopigwa ya kukubali kuhairisha michezo hiyo.
Michezo ya wiki ya 20 itakayoanza Desemba ilitarajiwa kuwa ingeahirishwa ili kupunguza presha, lakini klabu zimekubaliana kama wachezaji 13 wako sawa akiwamo kipa mchezo uchezwe.
Pia kuna mazunguzo kati ya klabu na mamlaka kuiondoa michezo ya Kombe la FA ya mzunguko wa tatu na nne na kuipunguza michezo ya nusu fainali ya EFL (Carabao Cup) kuchezwa mchezo mmoja tu na si miwili kama ilivyo kawaida.
Michezo mitano kati ya sita ya Jumamosi iliahirishwa, Chelsea waliomba nao mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Wolves uahirishwe na mamlaka ilikataa, pia Liverpool walikuwa miongoni mwa timu zilizotaka michezo ya wiki 20 kuahirishwa.