Kaimu Mtendaji Mkuu wa Young Africans, Senzo Masingiza Mbatha ameweka wazi kuwa mradi wao wa ujenzi wa Uwanja ambao unafahamika kwa jina la Kigamboni Complex ‘Home of Champions’ tayari umeshawapata wakandarasi ambao wataanza kazi muda wowote kuanzia sasa.

Senzo ameanika wazi mpango huo, baada ya Simba SC kutangaza mchakato wa kuchangisha fedha za ujenzi wa Uwanja wa kisasa ambao utagharimu Shilingi Bilioni 30.

Ijumaa (Desemba 17) Uongozi wa Simba SC uliweka hadharani mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa uwanja huo kupitia sehemu mbalimbali.

Senzo amesema: “Mradi tayari ulishapata wakandarasi wa kuuanza kufanya kazi ambapo muda wowote kuanzia sasa Kigamboni Complex Home of Champions itaanza kufanyiwa kazi jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa klabu yetu.

“Yanga tuna mipango mingi sana endelevu na bora kwa ajili ya klabu hivyo kuna vitu vingi sana vinatakiwa kukamilika ili watu waone maendeleo yenyewe,”amesema kiongozi huyo.

Herry Mzozo: Sure Boy amesaini Young Africans
Minziro: Kazi imeanza rasmi Geita Gold FC