Mwisho wa mwaka ndio kipindi ambacho mara nyingi kila mmoja hufanya tathmini yake juu mambo mbali mbali yaliyojiri kwa kipindi cha mwaka mzima, sasa kuelekea kuuhitimisha mwaka 2021.

Kutoka kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo fleva rapa Nay wa Mitego amefunguka tathmini yake juu ya muziki wa Hip Hop nchini.

Ni kupitia kwenye kipindi cha xxl kinachorushwa na na kituo cha radio cha clouds fm, Nay amebainisha mengi kuhusu thamani ya muziki huo.

Huku akitilia mkazo kuwa licha ya kutoonekana kupenya nje ya mipaka ya Tanzania kwa kasi kubwa ila bado muziki huo unaongoza kwa ukubwa kuliko muziki wa kuimba.

“Mwaka 2021 kwangu mimi kwenye Bongo fleva Kwa Tafsiri Ya haraka haraka muziki wa Rap Umekuwa mkubwa zaidi kuliko wa kuimba, ukiangalia mimi ndio msanii wa rap amabaye nimepeleka nyimbo tatu mfululizo Namba Moja kwenye trend,

Mimi ndio msanii wa rap nadhani nimeongeza namba nyingi kuliko msanii mwingine wa rap. Hii Ni tafsiri kubwa sana kwa muziki wa rap nchini.

Muziki wa rap una nguvu Kubwa kuliko wa kuimba japo kuwa marapa wengi wamechoka nadhani Wameamua kuikatia tamaa Rap” alisema Nay.

Kwa mujibu wa kauli ya Nay ni kuwa kutokana na kujikatia tamaa kwa baadhi ya wasanii wa muziki wa Hip Hop nchini ndio kama sababu ya kupatikana mwanya wa aina tofauti za muziki kuchukua sehemu fulani ya muziki.

“Nadhani wanaweza kujifunza kwa hiki ambacho nimekifanya kwa mwaka huu, muziki wa rap una nguvu sana, sasa hivi tungekua tunatoa tuzo za msanii bora wa mwaka wa rap.

Sidhani kama nitakosa kila tuzo japo kuwa nafahamu nisingewekwa kwenye vipengele lakini wananchi Wangenipa tuzo kwa sababu  nilichokifanya Kinaonekana” aliongeza Nay wa Mitego.

Nay wa mitego kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Hunijui’ aliutoa takribani siku mbili zilizopita, huku mapokezi yake yakiwa makubwa kiasi cha kuchumpa mpaka namba tatu kwenye orodha ya video zenye ku-trend kupitia mtandao wa Youtube.

Bobi Wine ampa 'suprise' mkewe
Jeshi la Polisi latoa tahadhari