Meneja wa FC Barcelona XAVI amesema amekosa furaha baada ya kikosi chake kushindwa kupata ushindi katika mchezo walioutawala na kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sevilla hapo juzi Jumanne (Desemba 21).

Katika mchezo huo Barca walistahili ushindi, kwani walipiga mashuti 15 katika kipindi cha kwanza yakiwa mengi zaidi kuliko timu yoyote kwenye Ligi ya Hispania La Liga msimu huu 2021/22.

Jules Kounde alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 64 baada ya kumrushia mpira usoni, Jordi Alba, lakini Barca walishindwa kutumia nafasi ya wapinzani wao kuwa pungufu.

Matokeo hayo yanamaanisha Blaugrana hao wameshinda mchezo mmoja tu kati ya nane ugenini, Xavi alionekana kuchanganyikiwa na matokeo hayo, kwani alitarajia kuondoka pale Andalusia akiwa na alama zote tatu, huku akionyesha kuridhishwa na kiwango cha timu.

“Tumepoteza pointi mbili; tulistahili kushinda, hata wakati tulipokuwa 11 dhidi ya 11,” amesema Xavi akiiambia Movistar.

“Itakuwa ngumu kwangu kulala kwa sababu tulitakiwa kushinda. Sevilla waliweza kutulia mchezoni na kuufanya sisi tuwe na wakati mgumu.”

Luis Miquissone atwaa CAF Super Cup
WHO yaonya chanjo ya nyongeza