Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Young Africans wamepangwa Kundi B kuelekea Michuano ya mwaka 2022 ambayo itaanza rasmi Januari 02.

Young Africans ilitwaa Ubingwa wa Michuano hiyo kwa kuifunga Simba SC kwa changamoto ya mikwaju ya Penati mapema mwaka huu mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Kamati Maalum ya Michuano hiyo ambayo ni sehemu ya Sherehe za Mapinduzi matukufu ambazo hufanyika Januari 12 kila mwaka, imepanga makundi matatu na Ratiba ya michuano hiyo.

Young Africans imepangwa Kundi B na timu za Taifa Jang’ombe na KMKM, huku Mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo Azam FC ikitupwa Kundi A sambamba na Namungo FC, Yosso Boys na Meli 4 City.

Simba SC ipo Kundi C lenye timu za Selem View na Mlandege FC.
Mchezo wa Ufunguzi utashuhudia Namungo FC wakipepetana dhidi ya Meli 4 City, huku Young Africans wakitarajia kuanza kutetea ubingwa wao Januari 05 kwa kucheza dhidi ya Taifa Jang’ombe.

Simba SC nayo itaanza kusaka Ubingwa wa Michuano hiyo Januari 05 kwa kucheza dhidi ya Selem View.

Rais Samia afanya uteuzi
Liverpool yapelekwa London, Chelsea kuivaa Spurs