Hatimaye, mratibu wa hafla ya tamasha la Bright Future lililofanyika takribani wiki moja iliyopita huko Mombasa nchini Kenya, amesema kuwa msanii Masauti aliiaibisha Mombasa nzima kwa kitendo cha kuchelewa kutumbuiza kwa  zaidi ya saa 2.

Hayo yameelezwa Baada ya Masauti kujitetea katika.mitandao ya kijamii akidai Makosa ni ya muandaaji.

Bianca, ambaye ni mtaalam wa mahusiano ya Umma aliyehusika katika tamasha hilo, aliamua kufichua kuwa timu yake ilijaribu kuwasiliana na Masauti ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyotokea baada ya kufanyika kwa makosa hayo tangu siku ya tukio.

“Masauti, watu kadhaa wamekupigia lakini umekataa kupokea simu. Tafadhali fanya kinachohitajika, achana na aibu,” aliomba Bianca.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Masauti na Nadia Mukami waliamriwa kutoka nje ya jukwaa bila ya kujali ili kutoa nafasi kwa msanii Mbosso kutoka nchini Tanzania kutumbuiza kwenye jukwaa hilo.

Siku ya Jumatano, Desemba 22, Masauti aliweka ujumbe wa wazi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram, akimlaumu promota wa onyesho hilo kwa misukosuko iliyojitokeza, na kulisafisha jina la Mbosso lililokuwa likitajwa mara kwa mara.

“Sijataka kuongelea issue ya show ya Mombasa lakini pia nimeona nivunje ukimya ili kuepuka unafki. Najua mashabiki zangu wanahofu kutaka kujua what exactly happened ndio singependelea mtu atumie jina langu kuelezea my side of the story.

Masauti alieleza zaidi kuwa vurugu hizo zilianza dakika 30 baada ya kupanda jukwaani kutumbuiza. “Nilifika kwenye location nikasubiri hadi mda wangu wa kupanda stage kuperform.

Baada ya kama nusu saa hivi, nikiendelea kuperform nikaona nyuma kuna mvutano unaendelea kati ya management yangu na watu kwenye stage. Yuleyule dada (Bianca) alitaka kunikatiza show katikati.”

Masauti alifichua kuwa chanzo cha kuchelewa kwake  ni promota wa onyesho hilo kuchelewa kuhangaikia usafiri wa kutoka hotelini ili kumrahisishia kufika kwa haraka kwenye onyesho hilo, licha ya kuwa walikuwa na makubaliano.

Ukitaka kuzaa na Huddah andaa Bilioni 2
Odinga asherehehekea Sikukuu na Watoto wahitaji