Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kumtafuta Mtume na Nabii Josephat Mwingira ili kumhoji juu ya tuhuma mbalimbali alizozitoa akiwa kanisani kwake
Simbachawene ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 27, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali.
Hatua hiyo ya Waziri Simbachawene imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikimnukuu Askofu Mwingira akitoa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutishiwa maisha zaidi ya mara tatu na mali zake kuteketezwa shambani kwake ikiwemo mauretania na vifaa vingine
“Nchi hii ni nchi ya amani, haiwezekani mtu aishi kwa shida na kukosa raha kipindi chote hicho alafu Leo amesubiri wakati wa sikukuu ndio aseme mambo mazito kama hayo, anasababisha watu wote kukosa amani lakini yeyeni kiongozi maarufu tuahitaji atusaidie” amesema Simbachawene
Katika hatua nyingine Mwingira amesema dada yake aliuwawa na polisi katika nyumba ya kulala wageni ambapo ni baada ya kutoa taarifa polisi kuwa anatishiwa maisha yake.
Askofu Mwingira amekaririwa akizungumza hayo kanisani kwake wakati wa ibada Jumapili Desemba 26, ambapo alieleza madhila aliyopitia wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tano.