Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 5704 katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru
Kwa niaba ya Rais Samia, waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene ametoa taarifa hiyo alizungumza na waandishi wa habari Leo tar 27 Disemba ofisini kwake jijini Dar es Salaam
Miongoni mwa wanufaika hao ni wale waliotumikia robo ya vifungo vyao na wawe wameingia gerezani kabla ya tarehe 9 octoba mwaka 2021
Wengine ni wenye magonjwa ya kudumu na wasioweza kufanya kazi, wazee, wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wanawake walioingia gerezani wkaiwa wajawazito na wenye watoto na wenye ulemavu wa mwili na akili.
Pia wafungwa ambao wametumikia kifungo kwa zaidi ya miaka 20 na kuendelea na wale waliopewa adhabu ya kuwekwa kizuizini na wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 15
“Msamaha huu haujahusisha wafungwa waliohukumiwa makosa kwa makosa ya kuua, kutaka kujiua na waliohukumiwa kunyongwa, walioua watoto na wanatumikia kifungo cha bodi ya PAROLE na kifungo cha nje, wale wanaotumikia kifungo kwa makosa ya Uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, utekaji, kuwapa mimba wanafunzi, kusafirisha binadamu, usafirishaji wa dawa za kulevya, kukutwa na viungo vya binadamu, ujangili na wizi wa fedha za Serikali” alisema Simbachawene
Msamaha huo umetolewa katika utaratibu wa kuelekea mwisho wa mwaka ambapo awamu zote zilizopita za urais zimekua zikifanya