Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amempongeza dereva wa lori, Sirizani Butau kwa Ushujaa na ujasiri wake wa kuokoa watu nane katika basi lililokuwa likiteketea moto baada ya kupata ajali, na ameahidi serikali itautambua mchango wake.

Katika ajali hiyo iliyotokea Siku ya Christmas Dereva huyo aliokoa Watu nane kutoka kwenye Basi lililokuwa likiteketea kwa moto baada ya kugongana na gari lililobeba mafuta.

Katika ajali hiyo watu wanne walifariki dunia.

“Nichukue fursa hii kumshukuru Sirizani Butau aliyeokoa watu kutokana na Ajali ya Mutare. Kama serikali tutamheshimu kwa kujitolea kwake.” Ameandika Rais Emmerson Mnangagwa

Rais Farmajo amsimamisha kazi Waziri Mkuu
Dube, Kangwa, Tigere kuikosa Simba SC