Rais wa Somalia anayemaliza muda wake Mohamed Abdullahi Farmajo anasema amemsimamisha kazi Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble, ambaye aliongoza mchakato wa uchaguzi, kufuatia madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Aidha agizo la Rais la kumsimamisha kazi Waziri Mkuu Roble lilikuwa limeweka shinikizo kwa Waziri wa Ulinzi kugeuza uchunguzi dhidi ya madai ya ubadhirifu wa ardhi ya umma na Jeshi la Taifa la Somalia.

Hata hivyo Roble bado hajatoa tamko lolote kuhusiana na uamuzi huo wa ofisi ya rais, lakini awali amekanusha madai ya wizi wa ardhi aliyosema yalilenga kuharibu sifa yake.

Mapigano kati ya Rais Farmajo na Waziri Mkuu Roble yamezua hofu kubwa na wasiwasi kuhusu kuzorota kwa utulivu wa Somalia katikati ya ghasia za baada ya uchaguzi.

Japan, Tanzania kuendeleza ushirikiano
Rais Mnagangwa ampongeza dereva wa lori