Mwanamuziki nguli wa muziki wa Kongo Lulendo Matumona, anayejulikana zaidi kwa jina la General Defao amefariki Dunia Jumatatu, Desemba 27, 2021 huko Douala, nchini Cameroon.

Kwa ugonjwa wa kisukari, japo taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema licha ya kisukari kifo chake kimechagizwa zaidi na maambukizi ya covid-19 aliyoyapata hivi karibuni.

General Def Defao amefariki akiwa na umri wa miaka 62 na ilikuwa atimize umri wa miaka 63 mnamo Desemba 31, 2021.

Umauti umemkuta akiwa mjini Douala nchini Cameroon ambako alipaswa kutumbuiza kwenye tamasha binafsi.

Lakini saa kadhaa kabla ya show, Defao alishikwa na wasi wasi akiwa katika chumba chake. Alipatwa na hali iliyompelekea kukaribia kukosa fahamu kwa muda mrefu hadi alipogunduliwa na watu wake wa karibu usiku sana akiwa katika hali ya kutatanisha.

Baada ya kubainika kuwa hali yake si shwari Mara moja alikimbizwa hospitali ya Laquintinie huko Douala ambako alifariki Jumatatu jioni.

Mara baada ya kutangazwa kwa kifo chake, wasanii kadhaa wa Kongo akiwemo Fally Ipupa, Barbara Kanam, Ferre Gola walieleza masikitiko yao kwa kupotea kwa mwimbaji huyo nguli.

Baada ya zaidi ya miaka kumi ya kuishi uhamishoni nchini Kenya, Defao alirejea nchini mwake DRC Agosti 4, 2019.

Moja ya ishara zake za kwanza ilikuwa  ni kwenda Necropolis wanapopaita katikati ya Mbingu na Dunia kuzulu Makaburi ya magwiji wenzie wa muziki wa Kongo kina Papa Wemba, Tabu Ley, King Kester Emeneya, Madilu System, pamoja na  Pépé Kallé.

Alifanya tamasha lake la kwanza baada ya  kurudi nyumbani kwao DRC.

Safari yake ya mwisho Afrika Magharibi wiki chache zilizopita. Ilikuwa Ouaga, Burkina, kwenye hafla ya sherehe ya Kundé 2021. Na mnamo Novemba 26, kwenye ukumbi wa Palais des Sports huko Ouaga 2021, Defao aliipaza sauti yake kwa mara ya mwisho akitumbuiza jukwaani.

Akiwa amevalia koti lenye mkufu mkubwa wa dhahabu uliokuwa ukimeta shingoni mwake, msanii huyo alionyesha kwamba bado alikuwa na uwezo wa kufanya kazi yake kwa wepesi wa enzi za ujana wake.

Jioni hiyo, Defao alitunukiwa tuzo yaa heshima kwa maisha yake yote.

Wahamiaji haramu 51 wakamatwa
Eric Omondi na Zuchu mambo yanaendelea