Jeshi la Polisi jijini Dodoma limewatia mbaroni wahamiaji haramu 51 raia wa Ethiopia na watu wawili raia wa Tanzania waliokuwa wakisafirishwa katika gari la mizigo wakitokea Kanda ya kaskazini kuelekea mikoa ya Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 28 jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Onesmo Lyanga amesema kuwa, watuhumiwa hao wamekamatwa tarafa ya Bereko Wilaya ya Kondoa wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T.593 AUE aina ya fuso likiendeshwa na Ignas Mgosi (23) mkazi wa Mafinga akisaidiwa na Jafari Idd (39) mkazi wa Arusha.

Amesema kuwa askari walipekua gari hilo na kuwakamata wahamiaji hao raia wa Ethiopia wakitokea Moshi Kilimanjaro kwenda Iringa, huku akielezea mbinu iliyotumika ni kuwaficha kwa turubai, 

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Kaimu Afisa Uhamiaji, Adam Mkuyu amesema wamejipanga kila kona kuhakikisha hakuna mhamiaji anaingia kinyemela.

Sambamba na hayo yote Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Onesmo ametoa wito kwa vijana wa kitanzania na madereva na wamiliki wa magari kuwa waache tamaa ya kufanya vitendo vya uhalifu kwa kuwa uhalifu haulipi.

Kauli ya Ndugai yapishana na ya Rais Samia
Defao afariki Dunia