Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania bara Klabu ya Simba SC umethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na Kiungo Ibrahim Ajibu kuanzia leo Alhamis (Desemba 30).
Simba SC imethibitisha taarifa za makubaliano ya pande zote mbili kwa kuweka taarifa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za klabu hiyo.
taarifa iliyosambazwa kupitia kurasa za Simba SC unasomeka: “Tunamshukuru Ajibu kwa namna alivyojitoa kupambana kwa ajili ya Simba, na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake.”
Hata Hivyo tayari Ibrahim Ajibu ameshajiunga na Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja, saa chache kabla ya kutolewa kwa ujumbe wa SC kwa Mashabiki na Wanachama.
Kiungo huyo ametambulishwa Azam FC na kukabidhiwa jezi namba 8 ambayo ataitumia katika kipindi chote ambacho ataitumikia klabu hiyo ya Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es salaam.