Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kingine cha miaka 6 kuanzia January 17, 2022.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Samia pia amemteua Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia(CFR).

Katika hatua hiyo hiyo amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre(AICC)

Pia Rais Samia ameteua Patience Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Uteuzi wa Balozi Muombwa na Balozi Begium ulianza rasmi tarehe 28 Disemba na uteuzi wa Kilanga ulianza rasmi tarehe 30 Disemba 2021.

Rais Samia atangaza rasmi uwepo wa kirusi cha Omicron Tanzania
Wanajeshi nane mali wafariki